• HABARI MPYA

  Saturday, January 10, 2015

  BAHANUZI AANZA KUNG’ARA POLISI APIGA BAO DAKIKA YA KWANZA TU MTWARA

  MSHAMBULIAJI Said Rashid Bahanuzi (pichani juu) leo ameifungia bao Polisi FC ikitoa sare ya 1-1 na Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Bahanuzi amechukuliwa kwa mkopo Polisi FC kutoka Yanga SC katika dirisha dogo Desemba na leo akicheza mechi yake ya pili, amefunga bao dakika ya kwanza baada ya misimu miwili migumu Jangwani.  Bao la Ndanda lilifungwa na Jacob Massawe dakika ya 16.
  Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, JKT Ruvu imeifunga mabao 2-1 Stand United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mchezo kati ya Mgambo Shooting na Ruvu Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAHANUZI AANZA KUNG’ARA POLISI APIGA BAO DAKIKA YA KWANZA TU MTWARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top