Mtibwa Sugar imepunguzwa kasi na JKT Ruvu baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Azam Complex Chamazi leo
MTIBWA Sugar imepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo.
Matokeo hayo yanairejesha Mtibwa kileleni baada ya kufikisha pointi 17, baada ya mechi tisa sawa na mabingwa watetezi, Azam FC- lakini timu ya Manungu inapandishwa kwa wastani wa mabao.
JKT Ruvu inafikisha pointi 17 pia baada ya mechi 11, lakini inabaki nafasi ya tatu mbele ya vigogo Yanga pointi 15 na Simba 12.
JKT ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya saba, mfungaji Samuel Kamuntu ambaye aliuwahi mpira uliotemwa na kipa Said Mohammed Kasarama.
Mtibwa walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 36, mfungaji Ame Ally aliyemalizia kwa kichwa kona iliyochongwa na Shijja Kichuya.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Coastal Union imelazimishwa sare ya bila kufungana na Polisi Moro Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo leo, Coastal Union imelazimishwa sare ya bila kufungana na Polisi Moro Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
0 comments:
Post a Comment