• HABARI MPYA

  Sunday, January 18, 2015

  HIZI NDIZO HASIRA ZA RONALDO KUMWAGANA NA ‘KICHUNA’ IRINA

  MWANASOKA Bora wa Dunia, Crisitano Ronaldo ameonyesha kutovurugikiwa kwa kuachana na mpenzi wake, mwanamitindo Irina Shayk kwa kuendelea kufanya vitu uwanjani na kuvunja rekodi.
  Saa kadhaa baada ya Mwakilishi wa Irina Shayk kuthibitisha mlimbwende huyo kumwagana na nyota huyo wa Real Madrid, Ronaldo amefanya kitu kipya cha kusisimua. 
  Jioni ya leo, Ronaldo ameipiku rekodi ya mabao ya gwiji wa zamani wa klabu hiyo, Raul aliyefunga mabao 87 ugenini katika mechi 271 za Ligi.
  Ronaldo and Shayk reportedly split because the Russian model refused to attend his mother's birthday
  Imebaki historia; Cristiano Ronaldo akiwa na Irina Shayk enzi za mapenzi yao moto moto

  Hiyo inafuatia Ronaldo kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya Getafe, na sasa anafiksiha mabao 89 nje ya nyumbani katika mechi 92 tu. 
  Ilitarajiwa kuwa wiki ngumu baada ya Ronaldo kumwagana na Irina, lakini mambo yanaonekana kuwa tofauti, Mreno huyo akionyesha anathamini zaidi kazi kuliko mapenzi. 
  Mwanamitindo huyo wa Urusi hakuhudhuria sherehe za Ballon d'Or mjini Zurich, Uswisi usiku ambao mpenzi wake huyo alitunukiwa tuzo hiyo na kana kwamba hiyo haitoshi, Irina amemzuia Ronaldo hadi ‘kumfolo’ kwenye Twitter.
  Former Manchester United man Ronaldo controls the ball while trying to hold of a challenge from Lago
  Crisitano Ronaldo akimiliki mpira katika ya mabeki wa Getafe leo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HIZI NDIZO HASIRA ZA RONALDO KUMWAGANA NA ‘KICHUNA’ IRINA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top