• HABARI MPYA

  Monday, January 12, 2015

  MTIBWA SUGAR YAPANIA KUENDELEZA UBABE KWA SIMBA SC

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  KOCHA wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime Silili Kianga amesema kwamba Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba SC kesho itakuwa ngumu, lakini watapambana ili washinde.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Mexime amesema kwamba katika siku za karibuni wamekutana na Simba SC mara tatu na kushinda mara mbili 4-2 na 1-0 na kutoka sare mara moja, 1-1, hivyo anaamini mchezo wa kesho utakuwa mgumu.
  “Hivi karibuni tumecheza na Simba SC mara tatu, kwanza katika Ligi tukatoka sare 1-1 Morogoro, tukacheza mechi ya kirafiki Chamazi, tukawafunga 4-2 na tukakutana nao katika mchezo wa kwanza hapa, tukawafunga 1-0,”.
  Kocha wa Mtibwa Sugar Mecky Mexime amepania kuendelea rekodi yake nzuri dhidi ya Simba SC

  “Naamini kabisa mchezo wa Fainali utakuwa mgumu kwa sababu na wao watataka kulipa kisasi, kwa kulitambua hilo na sisi tunajipanga vizuri kwa ajili ya kuendeleza rekodi nzuri dhidi yao,”amesema.
  Kesho itakuwa ni mara ya pili Mtibwa Sugar kukutana na Simba SC katika Fainali ya mashindano haya, baada ya awali kukutana mwaka 2008 na Wekundu wa Msimbazi wakaibuka vinara.   
  Mtibwa Sugar imewahi kutwaa Kombe la Mapinduzi mara moja, mwaka 2010 wakiifunga Ocean View katika Fainali, wakati mara mbili walifungwa katika Fainali 2007 na Yanga SC katika michuano ya kwanza ya Kombe hilo na 2008 mbele ya Simba SC.
  Wachezaji wa Mtibwa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuitoa JKU juzi katika Nusu Fainali

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAPANIA KUENDELEZA UBABE KWA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top