• HABARI MPYA

  Sunday, January 11, 2015

  MGAMBO YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0

  BAO pekee la Fully Maganga limeipa ushindi wa 1-0 Mgambo Shooting dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga jioni ya leo.
  Ushindi huo, unaifanya Mgambo sasa itimize pointi 12 baada ya kucheza mechi tisa, wakati Ruvu inabaki na pointi zake 11.
  Katika mechi za jana za Ligi Kuu, Ndanda FC ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Morogoro Uwanja wa Nangwnada Sijaona, Mtwara wakati JKT Ruvu iliifunga 2-1 na Stand United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MGAMBO YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top