• HABARI MPYA

  Thursday, January 22, 2015

  MESSI AIPA USHINDI BARCELONA DHIDI YA ATLETICO MADIRD

  BAO pekee la Lionel Messi limeipa ushindi mwembamba wa 1-0 nyumbani, Uwanja wa Camp Nou, Barcelona dhidi ya Atletico Madrid katika Robo Fainali ya kwanza ya Kombe la Mfalme Hispania.
  Messi alifunga bao hilo dakika ya 85 usiku wa kuamkia leo, baada ya kuuwahi mpira uliookolewa na Jan Oblak kufuatia mkwaju wa penalti alioupiga yeye mwenyewe na kuutumbukiza nyavuni.
  Penalti hiyo ilitolewa baada ya Juanfran kumchezea rafu Sergio Busquets na sasa timu hizo zitarudiana wiki ijayo katika Robo Fainali ya pili ya michuano hiyo Uwanja wa Vicente Calderon. Fernando Torres alianza jana katika kikosi cha Atletico, lakini akatolewa mapumziko kumpisha Mario Mandzukic.
  Lionel Messi (left) runs off in celebration after scoring the rebound having missed a penalty to put Barcelona ahead against Atletico Madrid
  Lionel Messi (kushoto) akikimbia kushangilia na Luis Suarez baada ya kuifungia bao pekee Barcelona dhidi ya Atletico Madrid

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2920515/Barcelona-1-0-Atletico-Madrid-Lionel-Messi-misses-penalty-scores-rebound.html#ixzz3PWDrlzEc 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI AIPA USHINDI BARCELONA DHIDI YA ATLETICO MADIRD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top