BONDIA Manny Pacquiao amependekeza pambano lake na Floyd Mayweather livutwe karibu baada ya kukubali vipengele vya mkataba na promota.
Mbabe huyo wa Ufilipino mwenye umri wa miaka 36, amekubaliana na kampuni ya Top Rank inayoandaa pambano hilo juu ya vipengele vya mkataba na sasa anasubiri na mpinzani wake naye, Mayweather afanye hivyo.
Taarifa za awali zinasema pambano hilo litafanyika Mei 2 mjini Las Vegas, Marekani baina ya mabondia hao wawili mahasimu wa miaka mingi.
Floyd Mayweather (left) may finally face Manny Pacquiao in the ring in May 2015
Rais wa Top Rank, Carl Moretti ameiambia ESPN.com: "Top Rank na Manny tumekubaliana vipengele kwa upande wetu. Sijui kuhusu upande mwingine,". Wiki iliyopita, Pacquiao aliliambia gazeti la Manilla Standard: "Tutatoa tamko kabla ya mwisho wa mwezi. Nafikiri litakuwepo (pambano),".
Mayweather anataka kupigana Mei 2, Jumamosi ambayo ipo karibu na sikukuu ya Cinco de Mayo, ambayo imekuwa ni utamaduni wake miaka ya karibuni.
Lakini tarehe hiyo pia ni ambayo imependekezwa kwa ajili ya pambano kati ya Miguel Cotto na Saul 'Canelo' Alvarez, ambalo litakuwa moja ya mapambano makubwa ya kihistoria mwaka huu baina ya mahasimu hao wa Puerto Rico na Mexico.
0 comments:
Post a Comment