• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  WILFRIED BONNY ATUA MAN CITY KWA PAUNI MILIONI 25

  MSHAMBULIAJI Wilfried Bony amekamilisha uhamisho wa dau nono kutoka Swansea kwenda kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City.
  Mpachika mabao huyo wa Ivory Coast, ambaye yupo na timu yake ya taifa kwa sasa kwa maandalizi ya Fainali za Mataifa ya Afrika, anajiunga na kikosi cha Manuel Pellegrini kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25 huku Pauni nyingine Milioni 3 zikiongezeka katika Mkataba huo wa zaidi ya miaka minne.
  Bony, mwenye umri wa miaka 26, amekubali mkataba wa miaka minne na nusu na atakuwa anavalia jezi namba 14, ambayo awali ilikuwa inavaliwa na Javi Garcia. 
  Wilfried Bony has joined Manchester City on a four-and-a-half-year deal. He will wear the No 14 shirt 
  Wilfried Bony amejiunga na Manchester City kwa mkataba wa miaka minne na kukabidhiwa jezi namba 14 
  The 26-year-old puts pen-to-paper on his deal with Premier League champions Manchester City 
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 hapa anasaini Mkataba wa kujiunga na Manchester City 
  Wilfried Bony (posing with Ivory coast president Sidy Diallo) has completed his move to Manchester City
  Wilfried Bony akiwa na Rais wa Ivory Coast, Sidy Diallo baada ya kukamilisha uhamisho wake Manchester City

  WAFUNGAJI BORA 2014 

  Wilfried Bony - 20
  Sergio Aguero - 18
  Yaya Toure - 17 
  Wayne Rooney - 16
  Edin Dzeko - 14 
  Daniel Sturridge - 13
  "Ni hisia babu kubwa kwangu, ni heshima kubwa kuwa hapa na ni changamoto kubwa,"amesema Bony akiwa mwenye furaha. 
  "Kama mchezaji wakati wote ni vizuri kuwa sehemu ya klabu kubwa duniani na ni fursa nzuri kwangu kuwa katika mazingira hayo – ninajivunia sana hilo,".
  "Najisikia faraja sana kusubiri zama hizi mpya zifike, ni babu kubwa. Nafikiri ni uamuzi babu kubwa kwangu - Manchester City ipo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Unakumbuka mwishoni mwa msimu uliopita nilisema kwamba kama ninataka kuhama, itakuwa kwenye timu inayoshiriki mashindano hayo, kwa sababu ni michuano mikubwa ambayo ninataka haswa kucheza na kushinda pia,:.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WILFRIED BONNY ATUA MAN CITY KWA PAUNI MILIONI 25 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top