• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  BAFANA BAFANA YAIFUMUA MALI 3-0 KIRAFIKI

  AFRIKA Kusini, Bafana Bafana imekamilisha maandalzi yake ya Fainali za Mataifa ya Afrika 2015 kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Mali Uwanja wa Stade Monedan mjini Libreville, Gabon, leo.
  Shukrani kwao wafungaji wa mabao hayo, Thulani Hlatshwayo dakika ya 37, Sibusiso Vilakazi 82 na Dean Furman dakika ya 85 waliofanya Afrika Kusini iendelee na rekodi yake ya kutofungwa chin ya kocha Shakes Mashaba.
  mchezo ujao wa Bafana Bafana utakuwa dhidi ya Algeria ufunguz wa Fainali za Mataifa ya Januari 19, wakati Mali wataanza na Cameroon mjini Malabo.
  Mali: S.Diakite; D.Diakite, Konate, Tamboura, Wague, Doumbia, Keita, Sylla, Sako, M.Yatabare, S. Yatabare
  Afrika Kusini: Mabokgwane; Nhlapo, Hlatshwayo, Ngcongca, Matlaba, Furman, Jali, Masango, Phala, Vilakazi, Ndulula.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAFANA BAFANA YAIFUMUA MALI 3-0 KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top