• HABARI MPYA

  Wednesday, January 14, 2015

  MABINGWA KENYA WATAKA UPINZANI TANZANIA

  Na Vincent Malouda, NAIROBI
  MABINGWA wa ligi kuu ya Kenya, Gor Mahia, wameweka mikakati ya kucheza na timu za ligi kuu ya Tanzania kama mojawapo ya maandalizi ya kushiriki mechi za klabu bingwa barani Afrika mapema mwezi ujao.
  Mwenyekiti wa klabu hiyo, hakimu Ambrose Rachier alithibitisha kwamba wanapanga mechi za kirafiki na timu za Kenya, Uganda na Tanzania.
  “Tutacheza mechi nyingi za kirafiki na timu tofauti kutoka humu nchini na hata nje ya nchi,” alisema.

  Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zasema kwamba viongozi wanapanga mechi kadhaa mjini Kampala, Uganda na vile vile Dar es Salaam, Tanzania.
  Tayari Lweza FC ya Uganda imetuma ombi la kuandaa mchuano wa kirafiki na mabingwa hao wa mara 14 wa ligi kuu ya Kenya pindi tu watakapofika Kampala.
  Gor chini ya kocha Msikochi Frank Nuttal imehairisha mechi ya kujipima nguvu dhidi ya wanabenki KCB iliyoratibiwa kusakatwa alasiri ya leo ugani City baada ya vijana wake Rishadi Shedu kutoa sababu Nuttal alisema ni za kueleweka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MABINGWA KENYA WATAKA UPINZANI TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top