• HABARI MPYA

  Thursday, January 01, 2015

  KIIZA ATUA FANJA YA OMAN

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  ALIYEKUWA mshambuliaji wa Yanga SC, Hamisi Kiiza ‘Diego’ atajiunga na Fanja SC ya Oman, imefahamika.
  Wakala wa wachezaji, Said Maaskary anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwa simu kutoka Oman, kwamba Fanja imekwishamalizana na Kiiza na anakwenda Muscat kusaini Mkataba.
  Maaskary amesema Kiiza atafika Muscat Ijumaa kusaini Mkataba na mara moja kuanza maisha mapya bara la Asia.
  Kiiza alitemwa Yanga SC katika dirisha dogo kumpisha mshambuliaji Mliberia, Kpah Sherman na awali alijaribu kwenda Mnyamar ambako hata hivyo hakufanikiwa.
  Hamisi Kiiza kushoto anakwenda kuanza maisha mapya Oman

  Kiiza aliichezea Yanga SC tangu mwaka 2012 akitokea Bunamwaya ya kwao, Uganda na katika kipindi chote hicho alikuwa tegemeo la mabao la timu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIIZA ATUA FANJA YA OMAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top