• HABARI MPYA

  Saturday, January 03, 2015

  KAGERA SUGAR WAIKAMATA YANGA SC LIGI KUU, JKT RUVU YAWAKALISHA COASTAL MKWAKWANI

  Na Mwandishi Wetu, TANGA
  BAO pekee la Samuel Kamuntu dakika ya 38, leo limeipa ushindi wa 1-0 JKT Ruvu dhidi ya wenyeji Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Ushindi huo, unaifanya JKT Ruvu itimize pointi 13 baada ya mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya tano, ikiiteremshia Coastal nafasi ya saba.
  Coastal inabaki na pointi zake 12, hivyo kupitwa na timu mbili, baada ya Polisi Moro pia kutoka sare ya bila kufungana na Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Jamhuri, Morogoro hivyo kutimiza pointi 13 na kupanda nafasi ya sita.   
  Samuel Kamuntu wa pili kushoto ameifungia bao pekee JKT Ruvu leo

  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting imelazimishwa sare ya bila kufungana pia na Kagera Sugar ya Bukoba Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
  Kagera Sugar inabaki nafasi ya nne, kwa kufikisha poniti 14 sawa na Yanga SC walio nafasi ya tatu, lakini Watoto wa Jangwani wanabaki juu kwa wastani wao mzuri wa mabao.
  Hata hivyo, Yanga SC imecheza mechi nane, wakati Kagera sawa na Polisi, Stand, Coastal, Ruvu Shooting na JKT Ruvu zimecheza mechi tisa moja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR WAIKAMATA YANGA SC LIGI KUU, JKT RUVU YAWAKALISHA COASTAL MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top