• HABARI MPYA

  Sunday, January 04, 2015

  ES SETIF YAMTUPIA VIRAGO ‘BAGGIO’

  Na Mwandishi Wetu, SETIF
  MABINGWA wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ES Setif ya Tunisia wameamua kusitisha Mkataba na mchezaji wao, Lazhar Hadj Aissa ‘Baggio’ (pichani kulia), baada ya kutoridhishwa na uwezo wake tangu ajiunge na timu hiyo.
  BIN ZUBEIRY inafahamu benchi la Ufundi la Setif limeamua kuvunja Mkataba na kiungo huyo mshambuliaji ili kumruhusu kwenda kutafuta timu nyingine kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.
  Na hatua hiyo imefuatia mchezaji huyo kushindwa kabisa kufanya vizuri katika timu hiyo inayotumia jezi za rangi nyeusi na nyeupe.
  Mwanasoka huyo wa Algeria mwenye umri wa miaka 30 ambaye amepewa jina la utani Baggio kutokana na staili yake ya nywele, awali alichezea timu za Qadsia, Sharjah SC na MC Alger.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ES SETIF YAMTUPIA VIRAGO ‘BAGGIO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top