• HABARI MPYA

  Sunday, January 04, 2015

  AL AHLY YAMTEMA KIUNGO WA BURKINA FASO

  Na Salum Esry, CAIRO
  KOCHA Mkuu wa Al Ahly, Juan Carlos Garrido amemtema kiungo mshambuliai wa kimataifa wa Burkina Faso, Moussa Yedan katika kikosi chake cha Ligi ya Mabingwa Afrika 2015.
  Klabu hiyo ya Misri itaanzia kwenye hatua ya 32 Bora katika Ligi ya Mabingwa baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ratiba ya michuano yake mwaka huu.
  Kocha huyo Mspanyola ameamua kumtema Yedan kikosi cha Al Ahly kufuatia taarifa Mburkinabe huyo ataondoka timu hiyo yenye maskani yake Cairo mwezi huu.
  Mussa Yedan ametemwa kwenye kikosi cha Al Ahly Ligi ya Mabingwa

  Garrido pia amewaacha Islam Roshdy, Sherif Abdel Fadel, Ahmed Khairy na Amr Gamal, ambao ni majeruhi wa muda mrefu.
  Kikosi kamili cha Merreikh Ligi ya Mabingwa ni makipa; Sherif Ekramy, Ahmed Adel na Mosad Awad, mabeki; Mohame Nagiub, Saad Samir, Basem Ali, Sabry Rahil, Hussien Al Sayed, Mohamed Hani na Sherif Hazem.
  Viungo ni Hossam Ghaly, Hossam Ashour, Abdallah Al Saied, Waled Soliman, Ramdan Sobhi, Mahmoud Hassan, Momen Zakrayia, Mohamed Rezk na Mohamed Nagi Gedo, wakati washambuliaji ni Emad Meteb, Ahmed Abdel Zaher na Salahdin Said.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY YAMTEMA KIUNGO WA BURKINA FASO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top