• HABARI MPYA

  Thursday, January 08, 2015

  AVRAM GRANT AMUITA MCHEZAJI HAKUTARAJIWA KIKOSI CHA MWISHO AFCON

  Na Mwandishi Wetu, ACCRA
  KOCHA Avram Grant amewastaajabisha wengi kwa kumuorodhesha mshambuliaji Mahatma Otoo (pichani kushoto) katika kikosi chake cha mwisho cha Fainali za Mataifa ya Afrika.
  Mchezaji huyo anayecheza Norway, Otoo alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Ghana msimu wa 2012/2013 na sasa anachezea Sogndal. 
  Alikuwa miongoni mwa wachezaji 31 walioitwa katika kikosi cha awali cha Ghana wiki iliyopita akinufaika na kutokuwepo kwa Majeed Waris.
  Waris ameenguliwa katika kikosi hicho cha AFCON 2015 kutokana na maumivu ya goti aliyoyapata akiichezea klabu yake, Tranzonspor dhidi ya Eskisehirspor katika ligi ya Uturuki wiki iliyopita.
  Black Stars iliifunga Olhanense ya Ureno mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki Jumatano na leo watacheza mechi nyingine dhidi ya Camburr SC ya Uholanzi kabla ya kuivaa SC Freiburg katika mchezo wa mwisho wa kujipima nguvu Januari 14.
  Avram Grant amemuita Mahatma Otoo katika kikosi chake cha mwisho cha AFCON

  Black Stars wataondoka kwenye kambi yao Hispania kwenda Equatorial Guinea siku tano kabla ya kucheza mchezo wao wa ufunguzi wa AFCON dhidi ya Senegal mjini Mongomo.
  Kikosi cha mwisho cha Ghana cha wachezaji 23 ni makipa; Razak Braimah (Mirandes, Hispania), Fatau Dauda (AshGold) na Ernest Sowah (Don Bosco, DRC), mabeki Harrison Afful (Esperance, Tunisia), John Boye (Erciyesspor, Uturuki), Jonathan Mensah (Evian, France), Awal Mohammed (Maritzburg, Afrika Kusini), Baba Rahman (Augsburg, Germany), Edwin Gyimah (Mpumalanga Black Aces, Afrika Kusini) na Daniel Amartey, (FC Copenhagen, Denmark).
  Viungo ni Rabiu Mohammed (Krasnodar, Urusi), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italia), Afriyie Acquah (Parma, Italia), Solomon Asante (T.P. Mazembe, DRC), Christian Atsu (Everton, England), Mubarak Wakaso (Celtic, Scotland), Andre Ayew (Olympique Marseille, Ufaransa), Frank Acheampong (Anderlecht, Ubelgiji) na washambuliaji Jordan Ayew (Lorient, Ufaransa), Asamoah Gyan (Al Ain, UAE), Kwesi Appiah (Cambridge United, England), David Accam (Chicago Fire, Marekani), Mahatma Otoo (Sogndal, Norway).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AVRAM GRANT AMUITA MCHEZAJI HAKUTARAJIWA KIKOSI CHA MWISHO AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top