• HABARI MPYA

  Thursday, January 08, 2015

  YANGA SC ‘YAMTALIKI RASMI’ JUMA KASEJA

  REKODI YA JUMA KASEJA YANGA SC 

  Yanga SC 3-2 KMKM (Kirafiki, alifungwa mbili Dar)
  Yanga 1-3 Simba SC (Mtani Jembe, alifungwa tatu Dar)
  Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki, hakufungwa)
  Yanga SC 3-0 Ankara Sekerspor (Ziara ya Uturuki, hakufungwa)
  Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki, alifungwa mbili)
  Yanga SC 7-0 Komorozine (Ligi ya Mabingwa, hakufungwa)
  Yanga SC 0-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa moja)
  Yanga SC 2-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu, hakufungwa)
  Yanga SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-2 Mgambo JKT (Ligi Kuu alifungwa mbili)
  Yanga SC 1-0 Chipukizi (kirafiki Pemba, hakufungwa)
  Yanga SC 2-0 KMKM (Kirafiki Zanzibar, hakufungwa)
  Yanga SC 0-0 CDA (Kirafiki Dodoma, hakufungwa)
  Yanga SC 1-0 Ambassador (Kirafiki, hakufungwa)
  Na Mwandishi Wetu, ZANZIBAR
  YANGA SC imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango Juma Kaseja, iliyemsajili kwa Sh. Milioni 40 Novemba 8, mwaka juzi.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amewaambia Waandishi wa Habari leo katika hoteli ya Zanzibar Ocean View visiwani hapa kwamba, hatua hiyo imefikiwa baada ya mchezaji huyo kuanza kujiengua katika timu.
  “Tumefikia uamuzi wa kuachana na Kaseja, baada ya yeye mwenyewe kuanza kujiengua katika timu,”amesema Muro.
  Mwishoni mwa mwaka jana, Kaseja aliwasilisha barua kwa mwajiri wake, Yanga SC kutoa taarifa ya kuvunja makataba wake, uliokuwa umebakiza mwaka mmoja.
  Katika barua yake, Kaseja alisema sababu ya kuvunjwa Mkataba huo ni kukiukwa kwa masharti yaliyokubaliwa wakati wa kusainiwa Novemba 8, mwaka jana.
  Barua ya Kaseja iliyotumwa kupitia wakili wake, Mbamba & Co Advocates, Kaseja imesema wakati wa kusainiwa Mkataba huo ilikubaliwa malipo ya Sh. Milioni 40 yafanyike kwa awamu mbili.
  Alisema awamu ya kwanza, alilipwa Sh. Milioni 20 baada ya kusaini Mkataba huo, na ikakubaliwa fungu lililobaki apatiwe Janauri 15, mwaka jana na kwa sababu malipo ya fedha ndio msingi wa Mkataba wenyewe, kushindwa kulipa fedha hizo kunaondoa uhalali wake.hivyo, Yanga SC baadaye ilikuja kusema imekwishamlipa fedha zake zote Kaseja na hana anachodai, ingawa kipa huyo alifungua madai mapya, akidai anachukiwa na kocha wa makipa, Juma Pondamali hivyo hana amani ya kufanya kazi. 
  Juma Kaseja ametemwa rasmi Yanga SC iliyomsajili kwa Sh. Milioni 40 Novemba mwaka juzi. Picha ya chini ni Jerry Muro leo wakati anatangaza kutemwa kwa kipa huyo hoteli ya Ocean View, Zanzibar  Kaseja pia alidai amekuwa haaminiki kwenye klabu hiyo mbele ya viongozi na baadhi ya wanachama, hivyo hajisikii kuendelea kufanya kazi Jangwani.  
  Katika kipindi cha mwaka mmoja wa kuwa kwake, Yanga SC, Kaseja ameidakia mechi 15 tu timu hiyo tangu amesajiliwa Novemba mwaka jana, akiwa kipa huru baada ya kuachwa Simba SC, kati ya hizo mechi tano zikiwa za Ligi Kuu na moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika.  
  Kwa ujumla katika mechi hizo, Kaseja amefungwa jumla ya mabao 10, yakiwemo matatu Yanga SC ikilala 3-1 mbele ya mahasimu, Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe Desemba 23, mwaka juzi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC ‘YAMTALIKI RASMI’ JUMA KASEJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top