TIMU ya taifa ya Algeria usiku wa kuamkia leo imeichapa Afrika Kusini mabao 3-1 katika mchezo wa Kundi C Fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea Equatorial Guinea.
Thuso Phala alianza kuifungia Bafana Bafana dakika ya tano, kabla ya Tokelo Rantie kugongesha mwamba mkwaju wa penalti ambao ungeipa Afrika Kusini bao la pili.
Thulani Hlatshwayo alijfunga dakika ya 67 kuipatia Algeria bao la kusawazisha, kabla ya Faouzi Ghoulam kufunga la pili na baadaye Islam Slimani akafunga la tatu dakika ya 83.
Algeria inapanda kileleni mwa kundi hilo, ikifuatiwa na Senegal ambayo mapema jana iliifunga Ghana mabao 2-1 katika.
Sifa zimuendee Moussa Sow aliyetokea benchi na kufunga bao la ushindi.
Sow alifumua shuti akipiga mpira wa mwisho kabla ya filimbi ya kumaliza mchezo na kufunga bao la ushindi, baada ya Mame Biram Diouf kusawazisha bao la mapema la Black Stars lililofungwa na Andrew Ayew kwa penalti.
Hayo ni matokeo machungu kwa kocha wa zamani wa Chelsea, Avram Grant katika mchezo wake wa kwanza akiwa kazini Ghana, ambayo sasa yanawaweka mabingwa hao wa zamani katika mazingira magumu kuingia hatua ya 16 Bora.
Islam Slimani akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la tatu
0 comments:
Post a Comment