• HABARI MPYA

  Tuesday, January 20, 2015

  KIHEREHERE MIRALLAS AGOMBEA PENALTI, AKOSA NA KUINYIMA USHINDI EVERTON

  TIMU ya Everton imelazimishwa sare ya bila kufungana na West Bromwich Albion usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Goodison Park.
  Lakini Everton watalia na Kevin Mirallas aliyepoteza nafasi pekee nzuri ya kuvuna pointi tatu, baada ya kukosa penalti.
  Tena, aling’ang’ania kwenda kupiga penalti hiyo akigombea dhidi ya Leighton Baines- lakini kiherehere chote akakosa. Mirallas alitolewa mapumziko nafasi yake akaingia Bryan Oviedo.
  Sasa, timu ya Roberto Martinez inafikisha mechi sita za Ligi Kuu ya England bila ushindi, wakati Tony Pulis amechukua pointi nne katika mechi mbili tangu aanze kazi Midlands.
  Mirallas was substituted at half-time by Everton manager Roberto Martinez and replaced by Bryan Oviedo
  Kevin Mirallas aligombea penalti, lakini akakosa na kuinyima ushindi Everton. Hasira za kocha Roberto Martinez alimpiga benchi mapumziko, akaingizwa Bryan Oviedo

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2917327/Everton-0-0-West-Brom-Toffees-extend-winless-run-six-games-Kevin-Mirallas-misses-penalty-following-argument-Leighton-Baines-spot-kick-Goodison-Park.html#ixzz3PK8UP2w9 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIHEREHERE MIRALLAS AGOMBEA PENALTI, AKOSA NA KUINYIMA USHINDI EVERTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top