• HABARI MPYA

    Tuesday, November 04, 2014

    SIMBA SC WAINGIA KAMBINI NDEGE BEACH KUSAKA DAWA YA USHINDI

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC inaingia kambini Ndege Beach Hotel jioni ya leo kwa maandalizi ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting mwishoni mwa wiki.
    Simba SC imecheza mechi sita bila kushinda hata moja ikitoa sare zote na Jumapili itajaribu kusaka ushindi wa kwanza kabla ya ligi hiyo kwenda mapumziko kwa takriban mwezi mmoja.
    Kocha Patrick Phiri anapambana kikamilifu kuhakikisha anapata ushindi Jumapili, ili kuwafurahisha waajiri wake, amabo tayari wamemtishia kumfukuza kazi.

    Uongozi wa Simba SC wiki iliyopita ulimpa Phiri mechi mbili ahakikshe timu inafanya vizuri, vinginevyo Mkataba wake utasitishwa na sasa Mzambia huyo anakabiliwa na presha hiyo.
    Akitoka kupokea angalizo hilo, Phiri alitoa sare nyingine ugenini na Mtibwa Sugar 1-1 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro Jumamosi.
    Katika sare zote, ukitoa ile ya 0-0 na mahasimu, Yanga SC, Simba SC iliongoza na kuruhusu wapinzani kusawazisha baadaye kuanzia 2-2 na Coastal Union na baadaye 1-1 mfululizo na Polisi Moro, Stand United, Prisons na Mtibwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAINGIA KAMBINI NDEGE BEACH KUSAKA DAWA YA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top