• HABARI MPYA

    Wednesday, June 18, 2014

    BRAZIL YASHIKWA, SARE 0-0, KIPA LA MEXICO LAOKOA MABAO HAYO HUWEZI AMINI

    WENYEJI Brazil, wamelazimishwa safe ya bila kufungana na Mexico katika mchezo wa Kundi A Kombe la Dunia uliomalizika muda mfupi uliopita.
    Brazil wakiongozwa na nyota wake, Neymar walicheza vizuri na kushambulia mno langoni mwa wapinzani wao hao wa Amerika Kusini pia, lakini wakakosa bahati ya kufunga.
    Timu hiyo inayofundishwa Luiz Felipe Scolari ilifanya jitihada nyingi za kufunga kwa kutengeneza nafasi nyingi, lakini sifa zimuendee kipa wa Mexico, Guillermo Ochoa, aliyeinusuru timu yake kwa kuokoa mabao mawili au matatu ya wazi mno. 
    Ulinzi mkali: Neymar akijaribu kuwatoka mabeki wa Mexico katika mchezo ulioisha kwa sare ya bila kufungana
    Sare hiyo inaiacha Brazil iendelee kuishi kileleni mwa kundi hilo baada ya kufikisha pointi nne, baada ya awali kuifunga Croatia 3-1.
    Kikosi cha Brazil kilikuwa: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Paulinho, Gustavo, Ramires/Bernard dk45, Oscar/Willian dk84, Neymar na Fred/Jo dk68.
    Mexico: Ochoa, Aguilar, Rodriguez, Marquez, Moreno, Layun, Herrera/Fabian dk76, Vazquez, Guardado, Giovani/Jiminez dk84, Peralta/Hernandez dk74.Rising to the occasion: Neymar gets above Rafael Marquez and sends a header towards goal
    Bao la wazi: Neymar aliruka hewani kupiga kichwa vizuri akimzidi Rafael Marquez
    Saving the day: Mexico goalkeeper Guillermo Ochoa keeps the ball out as Brazil come close
    Lakini kips wa Mexico, Guillermo Ochoa akaokoa
    Showboating: Home favourite Neymar keeps the ball in the air despite the attentions of Andres Guardado
    Neymar akimroka Andres Guardado
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BRAZIL YASHIKWA, SARE 0-0, KIPA LA MEXICO LAOKOA MABAO HAYO HUWEZI AMINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top