KUNA tetesi, mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC wanataka kufanya ziara Hispania kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya.
Mwaka jana Azam waliweka kambi ya karibu wiki mbili Afrika Kusini na wakapata mechi nne za maana za kujipima nguvu dhidi ya klabu za Ligi Kuu ya huko.
Walicheza na Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundwons, Moroka Swallows na Orlando Pirates, zote zikitumia wachezaji wao halisi wa vikosi vya kwanza.
Ziara ile iliisaidia Azam na haikuwa ajabu mwisho wa msimu wakawa mabingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza katika historia yao.
Waliokuwa wapinzani wao katika mbio za ubingwa msimu huu, Yanga SC ambao walikuwa wana kikosi bora zaidi miongoni mwa klabu za Ligi Kuu, wao walifanya ziara Uturuki kwa mara ya pili mfululizo na kucheza na vitimu vya Daraja la Nne na nyingine kutoka nchi ‘mufilisi’ kisoka zilizokuwa ziara huko pia.
Tukajionea, Yanga iliyomaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ilikuwa bora zaidi kuliko iliyomalizia mzunguko wa pili baada ya kutoka Ulaya licha ya kuongezewa nguvu na kocha mpya Hans van der Pluijm na mchezaji hodari Emannuel Okwi.
Ziara za Ulaya mara nyingi kwa timu zetu za Afrika ni kwa ajili ya kuwafurahisha wachezaji tu, lakini zaidi huwa hazinufaishi timu.
TP Mazembe wale unaweza kusikia wamekwenda kuweka kambi Ghana au Zambia- kwa nini hawaendi Ulaya na wao wana fedha pia?
Hakuna mtu ambaye hajui kama Azam FC ni klabu tajiri, inayomilikiwa na bilionea mkubwa Tanzania, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake.
Azam hawahitaji kupandisha wachezaji wake ndege kwenda Ulaya tu kwa sababu Simba na Yanga waliwahi kwenda huko- bali wanatakiwa wafanye chochote kwa kufikiria namna bora ya kuiandaa timu yao.
Azam baada ya usajili iliyoufanya inahitaji kipindi kisichoungua siku 40 za programu ya mazoezi ya kujiandaa na msimu, bila ya hata kucheza mchezo wowote wa kujipima nguvu.
Kuwajengea wachezaji uimara wa miili yao (physic) kabla ya mashindano kutasaidia mno kuwaepushia na kuumia kwa urahisi.
Azam wanahitaji kupata sehemu yoyote nzuri kwa ajili ya kambi tulivu ya kujiandaa na msimu, hata iwe hapa Tanzania au nchi jirani.
Taifa Stars iliwahi kuweka kambi Bulyanhulu, Shinyanga chini ya Mbrazil Marcio Maximo- kwa kweli kambi ile ilikuwa ina tija sana.
Na ilipokwenda Brazil kuweka kambi nyingine ndefu, iliporejea ikafungwa 4-0 na Senegal. Chini ya Maximo pia, Stars ilikwenda nchi za Scandinavia, iliporejea ikavurunda.
Simba SC walipitia Nice, Ufaransa mwaka 1993 kuweka kambi ya wiki moja wakati wanakwenda Algeria kumenyana na Al Harach katika Kombe la CAF.
Ile ilikuwa kambi sahihi, hali ya hewa ya Algeria na Ufaransa zinafanana na nchi ambazo zimepakana na ndiyo maana Simba SC waliitoa Harach.
Azam nao kama watapangiwa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika nchini Morocco, wanaweza kupitia Hispania kuweka kambi fupi kama Simba SC, kwa kuwa hizo pia ni nchi ambazo zimepakana na hali ya hewa inafanana.
Lakini pia, katika kupanga mambo yao, vyema viongozi wa Azam FC wakafikiria na kubana matumizi, kwa sababu hadi sasa Azam FC kama klabu bado haiingizi chochote.
Hakuna kambi ya siku 10 au ya wiki mbili ya kujiandaa na msimu na je, Azam watakuwa watayari kukaa Hispania kwa siku japo 30? Na vipi kuhusu hizo Gharama za kuiweka timu huko?
Hakika sioni kama Azam wanahtaji kambi ya Ulaya, zaidi ya kupata sehemu nzuri hata hapa hapa Tanzania, ambako wachezaji watalishwa mazoezi ya kuwajengea uimara kabla ya msimu.
Baada ya hapo, ili kupima uwezo wake inafanya ziara ya wiki moja katika moja ya chi yenye timu bora kucheza nazo mechi za kirafiki.
Lakini kama kuwafurahisha wachezaji wake kwa safari ya Ulaya, wasubiri ratiba yao Ligi ya Mabingwa Afrika ikitoka waangalie namna ya kuichomokea safari hiyo kama walivyofanya Simba SC 1993. Ni ushauri tu.

.png)
0 comments:
Post a Comment