| Rais Kikwete na Marie Frances jijini Washington DC |
Na Prince Akbar
MWASISI wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon Marie Frances
mji wa Bethesda nchini Marekani amemsifu Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama
kiongozi anayependa nchi yake na anayeona mbali. Marie Frances ametoa sifa hizo
hapa mjini Moshi wakati Rais Kikwete akikutana na viongozi wa Chama Cha Riadha
Tanzania (AT) kupanga mikakati ya kufufua riadha nchini hivi karibuni.
Ofisa Uhusiano wa Mt Kilimanjaro Marathon, Grace Soka
ameiambia BIN ZUBIRY kwamba Frances ambaye aliwahi kukutana na Rais
Kikwete wakati wa ufunguzi wa jengo la Tanzania House katika jiji la Washington
DC amesema kuwa ni nadra sana kuona kiongozi wa nchi akikutana na viongozi wa
chama cha mchezo wowote kuzungumzia maendeleo yake. Hii ni miujiza hata katika
nchi kama Marekani.
Marie Frances amemuelezea Rais Kikwete kama mtu wa haiba ya
kipekee mwenye akili na maono ya kuiendeleza Tanzania kufikia malengo ya Umoja
wa Mataifa ya Millenia. “Nilimpenda sana nilipokutana naye jijini Washington.
Ni kiongozi mwenye haiba ya kipekee” alisema Frances ambaye aliombwa na balozi
wa zamani wa Tanzania nchini Misri kuja kuanzisha mbio za marathon nchini
Tanzania mwaka 1990.
Marie Frances ambaye alikuwa mkuzaji (producer) wa Miss
Universe pamoja na vipindi vya television huko Hollywwod nchini Marekani
alihamia nchini Misri mwaka 1984 kuafanya kazi ya ABC kama mwandishi wa bahari.
Akiwa nchini Mirsi, Marie Frances alianzisha mbio za Pyramid Marathon pamoja na
Miss Universe ambazo ziitangaza sana nchi ya Misri. Ni wakati wa matamasha haya
balozi wa Tanzania nchini Misri wakati huo alipomwomba aje Tanzania kuanzisha
mbio za marathon ili kuitangaza Tanzania.
Frances alikuja Tanzania mwaka 1990 na kutaka kuanzisha mbio
za Mt. Meru Marathon lakini alipofika tu mjini Moshi alivutiwa sana na mlima
Kilimanjaro na hivyo kuiamua kuanzisha mbio za “Mt. Kilimanjaro Marathon” mwaka
1991. Mbio hizi hukimbiwa kila jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita na
zitatimiza miaka 22 tarehe 24 Juni mwaka
huu.
Mt. Kilimanjaro Marathon zimeshapewa tuzo mbalimbali kama
mbio za kimataifa. Gazeti la Wonders of the World lenye wasomaji zadi ya
million 5 limezipa nafasi ya 2 kama mbio nzuri za kushiriki. Wakati jarida la
kimataifa la Forbes limezipa nafasi ya kwanza kama mbio nzuri za kukimbia!
Marie Frances pia ameanza kuwapeleka wanariadha wa Tanzania kukimbia nchini
Marekani kwa kuwasaidia fedha za Visa za Marekani pamoja na tiketi za ndege
kama inavyoonyesha picha ambapo mkimbiaji Nelson Brighton anapewa pesa na
Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Benadetta Kinabo kwenda nchi Marekani mwezi
ujao kwa ufadhili wake.Kwa sasa mbio hizi hufadhiliwa na shirika la ndege la
Ethiopia.
Ni katika juhudi zake za kuutangaza mlima Kilimanjatro ndipo
Manispoaa ya Moshi ikaipa jina la Marie Frances Boulevard barabara ya zamani ya
Bustani Ale.
Mt. Kilimajaro Marathon itaanzia Moshi Klabu tarehe 24 Juni
saa kumi na mbili asubuhi ambapo mbio za kilometa 42, 21, 10 na 5
zitashindaniwa na watalii toka Marekani pamoja na wakimnbiaji toka Moshi na
Arusha.
Wakimbiaji wanajiandikisha kwa wingi Bristol Cottages hotel
iliyopo mkabala na benki ya Standard Chattered karibu na Kilimanjaro Hospital
katika Manispaa ya Moshi.


.png)
0 comments:
Post a Comment