Tetesi za Jumatano magazeti Ulaya (1)

MA UNITED WALITIA PINGU BEKI LA KIBRAZIL KUWAKATA MAINI CHELSEA

KLABU ya Manchester United inatarajiwa kumpa mkataba mpya beki wake Mbrazil, Rafael da Silva, mwenye umri wa miaka 21, ili kuwakata maini wapinzani wao katika Ligi Kuu ya England, Chelsea wanaomtolea macho.
KLABU ya Malaga inataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Dimitar Berbatov, mwenye umri wa miaka 31, baada ya kuwapo taarifa klabu yake itamtema msimu huu.
MSHAMBULIAJI wa Croatia, Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 26, amewaambia Everton watatakiwa kuwa na subira hadi baada ya Euro 2012 ili kuamua mustakabali wake.
Dimitar Berbatov
Berbatov anaweza kutua Malaga
KLABU ya Manchester City itatakiwa kutoa kiasi cha pauni Milioni 30 kuinasa saini ya mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 27.
KINDA la Manchester United, Zeki Fryers, mwenye umri wa miaka 19, anaweza kuondoka Old Trafford, kutokana na klabu za Tottenham, Newcastle na Burnley zote kuwa na nia ya kumsajili beki huyo wa kushoto.
KLABU ya Reading iko tayari kuongeza dau ili kumpata Pavel Pogrebnyak, mwenye umri wa miaka 28. The Royals wametoa ofa ya pauni Milioni 13 kwa mshambuliaji huyo wa Urusi.
KLABU ya Benfica wako tayari kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Nicklas Bendtner, mwenye umri wa miaka 24, baada ya kung'ara katika mechi kati ya timu yake ya taifa, Denmark dhidi ya Ureno.
KLABU bingwa Ulaya, Chelsea imepanga kukata dau la pauni Milioni 10 kwa ajili ya winga wa Wigan, Victor Moses, mwenye umri wa miaka 21 inayemtaka.
Nicklas Bendtner
Nicklas Bendtner anatakjwa na Benfica
KLABU ya Manchester United inamtaka winga wa Porto, James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 20, kama mbadala halisi wa Luis Nani.
KLABU ya Anzhi Makhachkala ya Urusi inataka kumsajili beki wa Liverpool, Martin Skrtel, mwanasoka wa kimataifa wa Slovakia mwenye umri wa miaka 27.
KOCHA wa QPR, Mark Hughes anafikiria kumbadili kijana mtukutu, kiungo Joey Barton, mwenye umri wa miaka 29, na Stephen Ireland, mwenye umri wa miaka 25.
MSHAMBULIAJI wa Blackburn, Yakubu, mwenye umri wa miaka 29, yupo kwenye mazungumzo na mabingwa wa Ligi Kuu ya China, mabilionea Guangzhou.

WATATU WASIMAMISHWA CHELSEA

MAOFISA watatu wa klabu ya Chelsea wamesimamishwa kufuatia taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambalo klabu ilitwaa Mei mwaka huu kupata hitilafu.
BEKI wa Bolton, Zat Knight, mwenye umri wa miaka 32, anajiandaa kusaini mkataba mpya Uwanja wa Reebok, licha ya timu hiyo kushuka daraja kutoka Ligi Kuu.
NYOTA wa Chelsea, Juan Mata amesema kwamba klabu yake imempa ruhusa kuchezea Hispania katika michuano ya Olimpiki ya mwaka huu Jijini London.

VAN PERSIE NDANI YA ITV...

WASHAMBULIAJI wa Ligi Kuu ya England, Robin van Persie na Darren Bent wanajiandaa kushiriki mfululizo wa vipindi vya  vipya vya Televisheni ya ITV viitwavyo Red Or Black.