• HABARI MPYA

    Sunday, June 28, 2026

    GHANA YAFUZU HATUA YA 16 LICHA YA KUCHAPWA 2-1 NA CROATIA


    TIMU ya Ghana imefanikiwa kutinga Hatua ya 32 Bora Fainali za Kombe la Dunia licha ya kuchapwa mabao 2-1 na Croatia usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi L Uwanja wa Lincoln Financial Field Jijini Philadelphia, Pennsylvania, Marekani.
    Mabao ya Croatia yalifungwa na viungo wake wanaocheza Italia, Petar Sucic wa Inter Milan, mzaliwa wa Bosnia & Herzegovina dakika ya 31 na Nikola Vlasic wa Torino dakika ya 83, huku bao la Ghana likifungwa na beki wa kati wa Pafos ya Cyprus, Derrick Luckassen mzaliwa wa Uholanzi dakika ya 73.
    Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi L, mabao ya kiungo wa Real Madrid ya Hispania, Jude Victor William Bellingham mwenye asili ya Kenya dakika ya 62 na mshambuliaji wa Bayern Munich ya Ujerumani, Harry Edward Kane dakika ya 67 yaliipa England ushindi wa 2-0 dhidi ya Panama Uwanja wa MetLife Jijini East Rutherford, f New Jersey, Marekani.
    Kwa matokeo hayo, England imeongoza Kundi L kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Croatia pointi saba na Ghana pointi nne n azote zinafuzun Hatua ya 32 Bora, huku Panama iliyopoteza mechi zote ikiaga mashindano.


    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GHANA YAFUZU HATUA YA 16 LICHA YA KUCHAPWA 2-1 NA CROATIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top