• HABARI MPYA

    Friday, September 09, 2016

    WAZIRI NAPE KUKAGUA OFISI ZA TFF KESHO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye (MB) kesho Jumamosi Septemba 10, anatarajiwa kutembelea Ofisi za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.
    Akiwa TFF kuanzia saa 4.30 asubuhi, Waziri Nape atazungumza na Mwenyeji wake Rais wa Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji pamoja na Sekretarieti kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari ambao TFF imeawaalika katika ziara hiyo.
    Waziri Nape Nnauye kesho atazuru Ofisi za TFF, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam

    Katika ratiba hiyo, Nape ataonyeshwa maendeleo ya michezo hususani mashindano yanayodhaminiwa na Kampuni ya Airtel na kuratibiwa na TFF ambako kwa mikoa mbalimbali iliyofanya vema, kesho timu za wanawake na wanaume zitacheza hatua ya nusu fainali kabla ya fainali za Jumapili ambazo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAZIRI NAPE KUKAGUA OFISI ZA TFF KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top