• HABARI MPYA

  Tuesday, September 06, 2016

  SIMBA SC NA RUVU SHOOTING KUCHEZWA ‘SHAMBA LA BIBI’ KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  UWANJA wa Uhuru ‘Shamba la Bibi’, zamani Taifa, Dar es Salaam utaanza kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuanzia kesho, imeelezwa.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Licas amesema kwamba mechi ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo itakuwa kesho kati ya Simba SC na Ruvu Shooting.
  “Napenda kuwafahamisha kuwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam umeanza kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza,”amesema.
  Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki kupisha mechi za mwisho za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
  Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, washindi wa Ngao ya Jamii, Azam FC watakuwa wageni wa Prisons wakati Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, washindi wa tatu wa Ligi Kuu msimu uliopita, Simba SC watamenyana na Ruvu Shooting na Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa wageni wa Ndanda FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA RUVU SHOOTING KUCHEZWA ‘SHAMBA LA BIBI’ KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top