• HABARI MPYA

  Monday, September 19, 2016

  KENYA YAPANGWA KUNDI LA 'HAWACHOMOKI' AFCON YA WANAWAKE

  TIMU ya taifa ya wanawake ya Kenya, Harambee Starlets imepabgwa Kundi B na washindi wa rekodi mara tisa, Nigeria, Ghana na Mali katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zinazotarajiwa kuanza Novemba 10 hadi Desemba 3 nchini Cameroon.
  The Starlets, ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza AFCON watakuwa na wakati mgumu katika kundi walilopangwa na wababe hao watatu.
  Kenya watamenyana na Mali katika mchezo wao wa kwanza kabla ya kuwavaa Super Falcons na kisha kumaliza na Ghana.
  Wenyeji, Cameroon watamenyana na Banyana Banyana ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza siku ya ufunguzi Novemba 19 Kundi A. Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Misri na Zimbabwe
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KENYA YAPANGWA KUNDI LA 'HAWACHOMOKI' AFCON YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top