• HABARI MPYA

    Friday, September 02, 2016

    GAMBIA WAIFUATA CAMEROON NA KIKOSI CHA CHAN ZAIDI

    KOCHA wa Gambia, Sang John Ndong amechukua wachezaji 10 wanaocheza nyumbani katika kikosi cha wachezaji 18 kwa ajili ya mchezo wa Kundi M kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Cameroon Jumamosi mjini Limbe.
    Beki wa Brikama United, Hamidou Bojang, ambaye huchezea timu za vijana ameitwa pamoja na Steve Biko mshambuliaji Pa Dodou Darboe. 
    Ndong atawakosa wachezaji tegemeo kama Modou Barrow wa Swansea City ya England ns mshambuliaji anayecheza China, Bubacarr Trawally baada ya wawili hao kujitoa kikosini.
    Mwingine atakayekosekana ni mchezaji mpya wa Genk, Omar Colley, ambaye alikuwa Nahodha wa Nge hao kwenye mechi mbili zilizopita za kufuzu dhidi ya Mauritania na Afrika Kusini; wakati Tijan Jaiteh na Dawda Ngum wamerejeshwa kikosoini.
    Nge hao walipoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Renaissance Sportive Berkane ya Morocco kwa kufungwa 1-0 kabla ya kwenda Limba wakipitia Douala jana usiku.
    Gambia ambayo haijashinda mechi, ina pointi mbili tu baada ya kucheza mechi tano na wanashika mkia kundini. Cameroon yenye pointi tisa inaongoza kundi ikifuatiwa na Mauritania yenye pointi saba moja zaidi ya Afrika Kusini.
    Kikosi kamili cha Gambia kinachomenyana na Cameroon kesho ni makipa; Modou Jobe (Niarry Tally, Senegal), Alagie Nyabally (Real de Banjul).
    Mabeki: Alieu Jatta (Génération Foot, Senegal), Bubacarr Sanneh (AC Horsens, Denmark), Mass Manga (Hawks), Nuha Barrow (Gamtel), Gregory Sambou (Ports Authority), Hamidou Bojang (Brikama United). 
    Viungo: Dawda Ngum (FC Holviken, Sweden), Ebou Kanteh ( Real de Banjul), Mustapha Carayol (Nottingham Forest, England), Tijan Jaiteh (KuPS, Finland), Lamin Charty (Hawks), Bully Drammeh (Real de Banjul), Sainey Sambou (Brikama United) 
    Washambuliaji: Lamin Jallow (Chievo Verona, Italy), Pa Dodou Darboe (Steve Biko), Assan Ceesay (FC Lugano, Switzerland).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GAMBIA WAIFUATA CAMEROON NA KIKOSI CHA CHAN ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top