• HABARI MPYA

  Wednesday, September 14, 2016

  DEO NJOHOLE ‘OCD’ ALIPOKUWA MCHEZAJI WA YANGA KJWA MUDA

  Beki hodari wa kati wa Simba, Deo Njohole ‘OCD’ (wa pili kulia) akiwa na wachezaji wa Yanga wakati wa mapumziko katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Uganda, The Cranes mwaka 1992 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Dar es Salaam. Njohole alitokea kambi ya timu ya taifa, Jeshi la Wokovu kwenda kuchezea Yanga kama mchezaji mwalikwa baada ya kushawishiwa na wachezaji wa klabu hiyo aliokuwa nao kambini Taifa Stars. Wengine pichani ni Lawrence Mwalusako (kulia), Wastara Baribari (mbele kabisa), Ramadhani Kilambo (kushoto) na Abubakar Salum ‘Sure Boy’ anayezungumza na Abbas Gulamali (sasa marehemu) aliyekuwa mfadhili wa klabu. Njohole hakuendelea kucheza Yanga baada ya mchezo huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DEO NJOHOLE ‘OCD’ ALIPOKUWA MCHEZAJI WA YANGA KJWA MUDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top