• HABARI MPYA

  Thursday, September 15, 2016

  AZAM YAMKWAMISHA KIPRE TCHETCHE KUCHEZA OMAN

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Kipre Herman Tchetche amekwama kuichezea Al-Nahda Al-Buraimi ya Oman kutokana na klabu hiyo kushindwa kumalizana na Azam FC ya Tanzania.
  Kipre Tchetche amerejea nyumbani kwao Ivory Coast, baada ya Al-Nahda kushindwa kuwapa Azam FC dola za Kimarekani 50,000 (zaidi ya Sh. Milioni 100) walizotaka kumuachia mpachika nabao huyo. 
  Kipre Tchetche alikuwa amebakiza mwaka mmoja katika Mkataba wake Azam FC na akaondoka bila ridhaa ya klabu yake hiyo baada ya kuichezea kwa miaka mitano.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YAMKWAMISHA KIPRE TCHETCHE KUCHEZA OMAN Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top