• HABARI MPYA

    Wednesday, November 16, 2016

    SIMBA B YAANZA NA MOTO LIGI YA VIJANA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Simba imeanza vyema Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 Tanzania Bara baada ya kuifunga Ndanda FC ya Mtwara mabao 2-1 katika mchezo kituo cha Dar es Salaam.
    Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, mabao ya Simba yalifungwa na Rashid Juma dakika ya 24 na Moses Kitandu dakika ya 57, wakati la Ndanda limefungwa na Joseph Hilly dakika ya 89 kwa penalti. 
    Mashabiki wa Simba wanafurahia timu zao kufanya vizuri katika Ligi ya Bara

    Katika mchezo uliofuatia Ruvu Shooting wameilaza 1-0 JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex pia. Bao pekee la Ruvu limefungwa na Salehe Likwayu dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati baada ya William Patrick kuchezewa rafu.
    Mechi ya ufunguzi jana, Yanga ilitoa sare ya 1-1 na wenyeji Kagera Sugar kituo cha Bukoba, Uwanja wa Kaitaba na kesho jioni Chamazi Majimaji itamenyana na Mtibwa Sugar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA B YAANZA NA MOTO LIGI YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top