• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 29, 2016

  KAMATI YA NIDHAMU TFF YAFUTA ADHABU ZA KAMATI YA SAA 72

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limefuta adhabu iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) kwa viongozi na wachezaji wa Kimondo.
  Kamati ya Saa 72, ilifanya tathmini ya mchezo huo Na. 23 kati ya Kurugenzi na Kimondo ambako iliamua kuwafungia viongozi wa Kimondo, Eric Ambakisye, Selestine Mashenzi, na Mussa Minga kwa miezi sita na kupigwa faini ya Sh. 500,000 kila mmoja.
  Walidaiwa kuwafuata waamuzi hotelini baada ya mechi ambapo walimpiga Mwamuzi Mussa Gabriel na kumjeruhi wakishirikiana na baadhi ya wachezaji ambao waliohusika katika tukio hilo wamefungiwa mechi sita na faini ya sh. 500,000 kila mmoja.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF,  Tarimba Abbas

  Wachezaji waliotajwa ni January Daraja Mwamlima, Daniel Douglas Silvalwe, Abiud Kizengo na Monte Stefano Mwanamtwa. Adhabu zote ni kwa mujibu wa Kanuni ya 24(6) ya Ligi Daraja la Kwanza.
  Hata hivyo, katika kikao chake Jumapili iliyopita, Kamati ya Nidhamu ya TFF, chini ya Mwenyekiti Tarimba Abbas ilikubaliana na hoja ya wapinga adhabu waliowasilisha malalamiko yao TFF mara baada ya kuadhibiwa na Kamati ya Saa 72.
  Hoja za viongozi wa Kimondo ni kuwa hakuwahi kuitwa mbele ya Kamati hiyo kuhusiana na jambo hilo kwa ajili ya kutoa utetezi wake na kuwa na shaka na kamati hiyo juu ya kutoa adhabu hiyo.
  Kamati ya Nidhamu ilikubaliana na hoja hizo na hivyo kufuta adhabu hizo na kuagiza kamati ya saa 72 ya Bodi ya Ligi Kuu kuandikia kamati ya Nidhamu kuhusu makosa hayo ili kusikilizwa upya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAMATI YA NIDHAMU TFF YAFUTA ADHABU ZA KAMATI YA SAA 72 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top