• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 26, 2016

  BALOTELLI KUKOSEKANA MECHI TATU NICE

  VINARA wa Ligue 1 Ufaransa, Nice watamkosa mshambuliaji wao, Mario Balotelli kwa angalau mechi tatu baada ya Mtaliano huyo kuumia mazoezini wiki hii, kocha Lucien Favre amesema.
  Balotelli aliumia sehemu ya nyuma ya mguu wakati wa mazoezi Jumanne na akakosa mechi Europa League Alhamisi timu yake ikifungwa 2-0 na Schalke 04, kipigo ambacho kinaitupa nje ya michuano hiyo The Azurean.
  "Hatakuwepo kwa mechi tatu zijazo katika siku 10 zijazo," amesema Favre na kuongeza; "Kwa mechi zitakazofuata hatujajua bado."
  Balotelli pia atakosa mechi ya nyumbani Jumapili dhidi ya Bastia, safari ya En Avant Guingamp na mechi nyingine ya nyumbani dhidi ya Toulouse.
  Habari nyingine mbaya ndani ya Nice ni kwamba kocha amethibitisha Paul Baysse, ambaye amekuwa nje ya Uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kucheza mechi tisa za ligi, will hatacheza hadi mwishoni mwa mwaka kwa sababu ya matatizo ya goti.
  Nice ina pointi 32 kutoka mechi 13 hivyo inaongoza ikiwazidi kwa pointi tatu Monaco wa pili na Paris St Germain wa tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BALOTELLI KUKOSEKANA MECHI TATU NICE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top