• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 24, 2016

  PRISONS YAMKANA MWAMBUSI, YASEMA WAO MEJA MINGANGE

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Prisons ya Mbeya umesema hauna mpango wala mkakati wa kufanya kazi na kocha wa Yanga, Juma Mwambusi.
  Kumekuwa na taarifa kwamba Mwambusi ataondoka Yanga kurejea Mbeya, safari hii akihamia timu ya Jeshi la Magereza, Prisons.
  Lakini akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Meneja na Msemaji wa Prisons, Enock Mwanguku amesema; “Si kweli”.
  Juma Mwambusi (kushoto) akiwa na bosi wake, Mholanzi Hans van der Pluijm (kulia)

  Amesema hadi sasa, hawajawa na mpango wa kubadilisha chochote katika benchi lao la Ufundi na wao wanastaajabishwa na uvumi wa kutaka kumchukua Mwambusi.
  “Hatuna mpango wa kumchukua Mwambusi na wala hatujawahi kuzungumza naye, nashangaa hizo habari sijui zinatoka wapi,”amesema Mwanguku.
  Mwanguku amesema hadi sasa Prisons iko chini ya kocha Meja Mstaafu, Abdul Mingange na huyo ataendelea na kazi.
  Prisons inatarajiwa kuanza mazoezi Novemba 26, mwaka huu kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Na Mwanguku amesema; “Timu yetu ni nzuri, tunaiamini, kama kuna mapungufu mwalimu atayafanyia kazi,”amesema.
  Mwambusi mwenyewe hakupatikana kwenye simu yake kuzungumzia juu ya kuzungumziwa kwake kuhamia Prisons akiwa bado ana Mkataba na Yanga.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PRISONS YAMKANA MWAMBUSI, YASEMA WAO MEJA MINGANGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top