• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 25, 2016

  ETO'O HATARINI KUFUNGWA MIAKA 10 KWA KUKWEPA KODI

  MWANASOKA Bora wa zamani Afrika, Samuel Eto'o yu hatarini kwenda jela zaidi ya miaka 10 kutokana na tuhuma za kukwepa kodi enzi zake anacheza Barcelona ya Hispania.
  Waendesha mashiaka pia wanataka Nahodha huyo wa zamani wa Cameroon alipe faini ya dola za KimarekaniMilioni 15.1 kwa makosa manne ya ukwepaji kodi ya Mamlaka ya Kodi Hispania kiasi cha zaidi ya dola Milioni 4 za Marekani kuanzia mwaka 2006 hadi 2009.
  Waendesha mashitaka wanataka hatua kama hizo zichukuliwe pia kwa mwakilishi wa wakati huo, Jose Maria Mesalles Mata.
  Samuel Eto'o yu hatarini kwenda jela zaidi ya miaka 10 kutokana na tuhuma za kukwepa kodi enzi zake anacheza Barcelona  

  Eto'o alicheza mechi 198 enzi zake Barcelona kuanzia mwaka 2004 hadi 2009, akifunga mabao 129 na kushinda mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa na matatu ya La Liga kabla ya kuhamia Inter Milan. Mshambuliaji huyo pia alicheza Ligi Kuu ya England katika timu za Chelsea na Everton.  
  Julai mwaka huu, Lionel Messi na baba yake walihukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kwa makosa ya kukwepa kodi, lakini hawakwenda jela kwa sababu hukumu ya kifungo cha chini ya miaka miwili mara ya kwanza kwa muhusika hafungwi nchini Hispania.
  Neymar na Barcelona pia wanakabiliwa na tuhuma kama hizo juu ya uhamisho wa mchezaji huyo kutoka kwao, Brazil. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ETO'O HATARINI KUFUNGWA MIAKA 10 KWA KUKWEPA KODI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top