• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 30, 2016

  MICHO AMBEBA JUUKO KIKOSI CHA UGANDA AFCON

  BEKI wa Simba ya Tanzania, Juuko Murshid ameitwa kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 40 wa Uganda kwa maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Gabon.
  Kocha wa Uganda, Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameiambaia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba amemuita Juuko kwa sababu ni beki mzuri na ana mchango mkubwa kwa The Cranes kufuzu AFCON ya mwakani.
  Micho amewataka wachezaji aliowaita katika kikosi  chake cha awali kuwa na mikipa; Onyango Denis, Odongkara Robert, Jamal Salim, Watenga Ismail, Ochan Benjamin.
  Mabeki ni Iguma Denis, Nsubuga Joseph, Wadada Nicholas, Ochaya Joseph, Batambuze Shafiq, Isinde Isaac, Juuko Murushid, Mukiibi Ronald, Awanyi Timothy, Kassaga Richard, Lwaliwa Khalid na Toha Rashid.
  Viungo ni Aucho Khalid, Mawejje Tony, Waswa Hassan, Azira Mike, Kizito Geoffrey, Kizito Keziron, Mutyaba Muzamil, Mugerwa Yassar, Sadam Juma, Oloya Moses, Kizito Luwaga Wiliam, Walusimbi Godfrey, Mucurezi Paul, Kiiza Martin na Vitalis Tabu. 
  Washambuliaji ni Miya Farouk, Massa Geoffrey, Serunkuma Geofrey, Shaban Mohamed, Sentamu Yunus, Nsibambi Derrick, Lubega Edrisa na Sekisambu Erisa.
  Micho amesema kikosi hicho kinaingia kambini mara moja kuanza maandalizi ya fainali za kwanza za AFCON kwa Uganda baada ya miaka 39.
  “Tumeita wachezaji 40 – makipa watano, mabeki 12, viungo 15 na washambuliaji wanane ambao watawania nafasi 23 za kikosi cha mwisho kitakachoiwakilisha Uganda AFCON ya kwanza baada ya miaka 39,”alisema Micho na kuongeza; “Tumechagua mseto wa wachezaji wa wazoefu na chipukizi ambao wamebeba mustakabali wa soka ya Uganda,”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MICHO AMBEBA JUUKO KIKOSI CHA UGANDA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top