• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 29, 2016

  KASEJA, BANKA WAJITOA TIMU YA TAIFA YA UFUKWENI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu unaochezwa ufukweni (Beach Soccer), John Mwansasu amesema anatafuta wachezaji wa kuziba pengo la kipa Juma Kaseja na kiungo Mohammed Banka. 
  Mwansasu anafuatilia viwango vya wachezaji mbalimbali ili kujaza nafasi moja ya kipa kabla ya Desemba mosi, 2016 baada ya Kaseja na Banka kujitoa.
  Kaseja amesema atakuwa na udhuru wakati Banka ameripotiwa kuwa safarini nchini Afrika Kusini.
  Kwa sasa Mwansasu ameita kikosi cha wachezaji 12 kati ya 13 wanaotarajiwa kuivaa Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Desemba 9, 2016 utakaofanyika Dar es Salaam.
  Mwansasu ambaye hivi karibuni kikosi chake kilicheza na Ivory Coast katika michezo miwili ya  kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni bila mafanikio ni makipa  ambao ni  Rajab Galla na Khalifa Mgaya.
  Mabeki ni Roland Revocatus, Juma Ibrahim, Kashiru Salum na Mohammed Rajab wakati Viungo ni Mwalimu Akida, Ahmada Ali na Samwel John huku washambuliaji wengine wakiwa ni Kassim Kilungo na Talib Ally pamoja na Ally Rabbi ambaye ni Nahodha na Mshambulaji wa timu hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KASEJA, BANKA WAJITOA TIMU YA TAIFA YA UFUKWENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top