• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 26, 2016

  WAYNE ATAKA KUONDOKA AZAM AKACHEZE KWA MKOPO KUPATA UZOEFU

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIUNGO chipukizi wa Azam FC, Omar Wayne ameomba kutolewa kwa mkopo timu nyingine ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ili akapate uzoefu.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana, Wayne alisema kwamba baada ya kujiridhisha kwamba hawezi kupata nafasi ta kucheza Azam FC kwa sasa chini ya kocha Mspaniola, Zeben Hernandez Rodriguez anaomba kutolewa kwa mkopo.
  Alisema lengo la kuomba kutolewa kwa mkopo timu nyingine ni ilia pate nafasi ya kucheza pamoja na kujikusanyia uzoefu ambao baadaye unaweza kuinufaisha klabu yake, Azam FC.
  Omar Wayne (kushoto) anaomba kutolewa kwa mkopo timu nyingine ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ili akapate uzoefu

  “Mimi ninaomba uongozi unitoe kwa mopo timu yoyote itakayokuwa kunisajili ili nipate nafasi ya kucheza, nipate uzoefu ili na mimi nikuze uwezo wangu kuliko hivi ninavyokaa Azam bila kucheza.
  Wayne alisema kwamba anaamini akitolewa kwa mkopo timu nyingine ya Ligi Kuu atapambana kugombea namba na kupata nafasi ya kucheza, kuliko hali ilivyo sasa Azam FC.
  Alisema Azam FC ina wachezaji wengi kuanzia Akademi hadi timu ya wakubwa na ushindani pia mkubwa wa namna, hivyo ili kwa wachezaji wadogo inakuwa ngumu kwao kupata nafasi.
  “Lakini mimi nina matumaini makubwa nikipata nafasi ya kucheza siku moja nitarudi Azam kishujaa. Kwa sababu naamini uwezo wangu na ndiyo maana napigania kutolewa kwa mkopo,”alisema.
  Omary Wayne alikuwa nahodha wa kikosi timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2014 wakati huo akiwa mchezaji wa Azam akademi.
  Mwaka jana alitolewa kwa mkopo Maji Maji na baadaye African Sports ya Tanga kabla ya Julai mwaka huu kuitwa kwa majaribio AmaZulu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, ambako pamoja na kufuzu, lakini klabu hiyo haikuwa tayari kuvunja mkataba wake na Azam FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAYNE ATAKA KUONDOKA AZAM AKACHEZE KWA MKOPO KUPATA UZOEFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top