• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 30, 2016

  MTIBWA SUGAR YASAJILI KIFAA CHA ZENJI

  Na Mwandishi Wetu, MOROGORO
  MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wameendelea kujiimarisha kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu baada ya kumsajili mchezaji mpya, kiungo Saleh Khamis Abdallah (kushoto) kutoka Zanzibar.
  Kocha wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga amesema leo kwamba, mchezaji huyo amekwishajiunga na wenzake kambini mjini Morogro kwa mazoezi.
  “Ni mchezaji mzuri, tunampa nafasi ya kujichanganya na wenzake ili wazoeane aweze kujisikia yupo nyumbani,”alisema Mayanga.
  Na mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa, Mayanga alisema kwamba wanatarajia Abdallah ni ingizo jipya litakalokuwa na tija  katika timu.
  Kikosi cha Mtibwa Sugar kinaendelea kujiwinda na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu katika uwanja wake wa nyumbani Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro kwa wiki ya pili sasa.
  Na kuhusu maandalizi ya timu kwa ujumla, Mayanga alisema; “Kwa kweli vijana wako vizuri na programu yangu inaenda vizuri na tunataka mzunguko wa pili tuwe kati ya timu bora,”.
  Mtibwa Sugar ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa katika nafasi ya tano kutokana na pointi zake 23, ikizidiwa pointi 10 na mabingwa watetezi, Yanga na pointi 12 na vinara, Simba SC.
  Na ikumbukwe Mtibwa Sugae iliuanza msimu huu kwa pigo kubwa, baada ya kuondokewa na wachezaji wake watatu nyota, Shizza Kichuya, Mohammed Ibrahim na Muzamil Yassin waliojiunga na Simba SC. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YASAJILI KIFAA CHA ZENJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top