• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 27, 2016

  ULIMWENGU: MIPANGO YA ULAYA INAENDELEA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu amesema yuko kwenye mazungumzo na wawakilishi wa klabu moja ya Ligi Kuu Ulaya na mambo yatakapokamilika ataweka hadharani.
  “Kaka mapema sana kuzungumza chochote, kwa sababu bado hatujafikia maafikiano. Ndiyo tupo kwenye mazungumzo na hawa Wazungu, acha tumalizane nao kabisa ndiyo tuweke mambo wazi,”alisema Ulimwengu akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo.
  Ulimwengu yupo nchini tangu mapema mwezi huu baada ya kuhitimisha miaka yake mitano ya kuitumikia klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na sasa anashughulikia mipango ya kuhamia Ulaya.
  Ulimwengu amesema yupo kwenye mazungumzo na wawakilishi wa klabu moja ya Ulaya

  Na kwa kipindi chote hicho amekuwa akifanya mazoezi makali ya kukimbi mchangani ufukweni, gym na kucheza mpira na timu yake mtaani ili kujiweka fiti wakati akisubiri kusaini timu nyingine.  
  Ulimwengu aliyezaliwa Juni 14, mwaka 1993 aliibukia katika taasisi ya soka Tanzania (TSA) mwaka 2008, kabla ya mwaka 2009 kwenda kuanza kukomazwa Ligi Kuu katika klabu ya Moro United alikokuwa akicheza kwa mkopo hadi mwaka 2010 alipokwenda akademi ya Athletic FC ya Sweden, alikocheza hadi 2011 TP Mazembe alipochukuliwa na timu ya vijana ya Mazembe.
  Alicheza U20 ya Mazembe kwa msimu moja kabla ya kupandishwa rasmi timu ya wakubwa mwaka 2012 na moja kwa moja kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza hadi anamaliza Mkataba.
  Ulimwengu anajivunia kushinda mataji makubwa akiwa na Mazembe kama Ligi ya Mabingwa Afrika, Super Cup ya Afrika na pamoja na kucheza Klabu Bingwa ya Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ULIMWENGU: MIPANGO YA ULAYA INAENDELEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top