• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 25, 2016

  SAMATTA AISAIDIA GENK KUFUZU MTOANO EUROPA LEAGUE

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana ametokea benchi na kuisaidia timu yake, KRC Genk kushinda 1-0 dhidi ya Rapid Viena katika Kundi F Europa League Uwanja wa Laminus Arena, Genk.
  Kwa matokeo hayo, Genk inafuzu hatua ya mtoano baada ya kupaa kileleni mwa Kundi F kwa pointi zake tisa, sawa na Athletic Bilbao ya Hispania. Genk inaongoza kwa wastani wa mabao, wakati Rapid Viena inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake tano sawa na Sassuolo ya Italia inayoshika mkia.
  Zikiwa zimesalia mechi moja moja kufunga hatua ya makundi, Rapid Viena na Sassuolo kwa vyovyote sasa haziwezi kuzipiku Genk na Bilbao.
  Samatta aliingia uwanjani dakika ya 85 kuchukua nafasi ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis katika mchezo ambao bao pekee la Genk lilifungwa na mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis dakika ya 11.
  Mbwana Samatta jana ameivusha KRC Genk hatua ya mtoano michuano ya Europa League  

  Huo unakuwa mchezo wa 34 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 14 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
  Katika mechi hizo, ni 17 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tano msimu huu, wakati 16 alitokea benchi nane msimu uliopita na 13 msimu huu – na mechi 10 hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu.
  Kikosi cha KRC Genk jana kilikuwa: Bizot, Castagne, Brabec, Colley, Nastic, Ndidi, Pozuelo, Susic/Heynen dk77, Bailey, Buffalo/Trossard dk89 na Karelis/Samatta dk85.
  Rapid Viena: Novota, Sonnleitner, Schösswendter, Dibon, Grahovac, Schaub/Jelic dk83, Schrammel, Traustason, Joelinton/Schobesberger dk62, Thurnwald/Kvilitaia dk72 na Wober.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AISAIDIA GENK KUFUZU MTOANO EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top