• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 29, 2016

  NUSU FAINALI KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA KWA WANAWAKE LEO

  NUSU Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake zinachezwa leo wenyeji Cameroon wakimenyana na Ghana mjini Yaounde wakati mabingwa watetezi, Nigeria wakimenyana na Afrika Kusini mjini Limbe.
  Nahodha wa Banyana Banyana, Janine van Wyk amesema kwamba mechi yao na Nigeria leo itakuwa vita
  Afrika Kusini walifika Nusu Fainli baada ya kuifunga Misri 5-0 kwenye mechi yao ya mwisho ya Kundi Group A na kumaliza nafasi ya pili hivyo kujipatia nafasi ya kukutana na vinara wa Kundi B, Nigeria, waliokusanya ponti saba katika mechi tatu.
  Banyana Banyana haijawahi kutwaa Kombe la Afrika na Van Wyk, ambaye ni mchezaji aliyeichezea mechi nyingi nchi yake, 140 anahisi huu ndiyo wakati wa kubeba taji hilo.
  Kocha Mkuu wa Cameroon, Enow Ngachu kwa upande wake amesema mchezo na Ghana utakuwa mgumu, lakini watapambana kupata matokeo mazuri ili wafike fainali.

  "Nimefurahishwa na uchezaji wa timu yangu hadi sasa. Tumepambana vizuri hadi kufika hapa, na sasa tunaingia kwenye Nusu Fainali kwa nguvu zetu zote,"alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NUSU FAINALI KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA KWA WANAWAKE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top