• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 28, 2016

  AZAM FC YAMTEMA MUIVORY COAST MWINGINE

  Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imemuacha mshambuliaji Muivory Coast, Ya Thomas Renaldo iliyemsajili mwanzoni msimu baada ya kusajili washambuliaji watatu kutoka Ghana. 
  Mapema mwezi huu, Azam FC iliwasaini washambuliaji Samuel Afful, Daniel Atta Agyei na Yahaya Mohammed wote kutoka Ghana.
  Na ili kubaki na wachezajin saba wa kigeni kwa mujibu wa kanuni, Azam imewatema Waivory Coast wote, beki Serge Wawa, kiungo Kipre Michael Balou na mshambuliaji Renardo walioingia timu hiyo kwa wakati tofauti.
  Ya Thomas Renaldo (kushoto) aliyesajiliwa mwanzoni msimu huu Azam FC ameachwa baada ya kusajiliwa Waghana watatu 

  Balou alitangulia mwaka 2011 pamoja na pacha wake, Kipre Herman Tchetche ambaye mwanzoni mwa msimu alihamia Oman alikokwenda kujiunga na klabu ya Al Suwaiq, wakati Wawa alifuatia mwaka 2014, wakati Renaldo alisajiliwa Julai mwaka huu.  
  Afful, Agyei na Mohammed wanafanya idadi ya wachezaji wa Ghana kufika wane, baada ya beki Daniel Amoah aliyesajiliwa Agosti.
  Hao wanaungana na kiungo Jean Baptiste Mugiraneza kutoka Rwanda na Wazimbabwe wawli, winga Bruce Kangwa na mshambuliaji Francesco Zekumbawira kukamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni.
  Kikosi cha Azam FC kwa sasa kipo kwenye mapumziko ya wiki mbili hadi Desemba 3 mwaka huu, kitakapoanza mazoezi ya kwanza kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na kombe la Shirikisho Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC YAMTEMA MUIVORY COAST MWINGINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top