• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 26, 2016

  SAMATTA: NIKO KATIKA WAKATI MGUMU KWA SASA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba yupo katika wakati mgumu kwa sasa na anahitaji kupambana kurudisha nafasi yake katika klabu ya KRC Genk.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Samatta amesema kwamba kwa sasa amekuwa akiingia dakika za mwishoni kutokana na mshindani wake wa namba, Nikolaos Karelis kufanya vizuri zaidi yake.
  Samatta amesema katika wakati mgumu kwa sasa na anahitaji kupambana kurudisha nafasi yake katika klabu ya KRC Genk

  Tunayecheza naye nafasi moja anafanya vizuri, Nico Karelis yuko kwny fomu nzuri anafunga karibu kila mechi, kwa hiyo anastahili kuanza mechi,”amesema Samatta leo akizungumza kwa simu kutoka Ubelgiji.        
  Hata hivyo, makali ya Samatta yalianza kupungua baada ya kuumia kwenye mchezo wa Europa League dhidi ya Rapid Wien ya Austria Septemba 15, mwaka huu Genk ikishinda 3-2 Uwnja wa Laminus Arena.
  Na siku hiyo, Samatta alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia na kutoka dakika ya 78, nafasi yake ikichukuliwa na Mbelgiji Karelis. 
  Samatta alikaa nje kwa wiki tatu na tangu hapon hata baada ya kurejea hajapata nafasi ya kuanza kutokana Karelis kufanya vizuri.
  Hadi sasa Samatta amecheza mechi 34 tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 14 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
  Katika mechi hizo, ni 17 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tano msimu huu, wakati 16 alitokea benchi nane msimu uliopita na 13 msimu huu – na mechi 10 hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na nne msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA: NIKO KATIKA WAKATI MGUMU KWA SASA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top