• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 22, 2016

  WALIOINGIA FAINALI MWANASOKA BORA AFRIKA NI HAWA

  MWANASOKA Bora wa Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borrusia Dortmund ya Ujerumani, atatetea tuzo yake dhidi ya Waalgeria wawili, Riyad Mahrez na Islam Slimani wote wa Leicester City ya England.
  Hiyo ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutoa orodha ya wachezaji watano wa mwisho wa kuwania tuzo hiyo. 
  Wengine wawili wanaowania tuzo hiyo ni Sadio Mane wa Senegal na Liverpool na Mohamed Salah wa Misri na Roma baada ya kupigiwa kura na Wajumbe wa Kamati ya Habari ya CAF, Kamati ya Ufundi na Maendeleo na nusu ya Wajumbe 20 maalum (Wajumbe 10).
  Katika kinyang'anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, ambayo inashikiliwa na Mtanzania Mbwana Samatta wachezaji wanne wa Mamelodi Sundowns wameingia fainali.
  Hao ni Khama Billiat wa Zimbabwe, Keegan Dolly, Hlompho Kekana wa Afrika Kusini na Denis Onyango wa Uganda ambao watachuana na mchezaji mmoja wa TP Mazembe, Rainford Kalaba wa Zambia.
  Katika hatua ya mwisho kura zitapigwa na Makocha wakuu wa timu za taifa za nchi 54 wanachama wa CAF, zikiwemo wanachama washifiki kama visiwa vya Reunion na Zanzibar pamoja na Wajumbe 10 maalum.
  Usiku wa tuzo za CAF 2016 utafanyika Januari 5, mwaka 2017 mjini Abuja, Nigeria chini ya udhamini wa kampini ya simu ya Globacom.
  Samatta hajaingia kutetea tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika kwa sababu alihamia KRC Genk ya Ubelgiji mapema mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WALIOINGIA FAINALI MWANASOKA BORA AFRIKA NI HAWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top