• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 28, 2016

  WACHEZAJI MBEYA CITY WAANZA KUKUSANYIKA KWA KAMBI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAKATI  mazoezi ya kipangwa kuanza kesho kutwa, baadhi ya nyota wa kikosi cha Mbeya City fc  waliokuwa nje ya jiji la Mbeya wanatarajia kuanza kuwasili  hii leo tayari kwa kuanza matayarisho ya duru ya pili ya ligi kuu ya  Vodacom Tanzania bara iliyopangwa kuanza kutimua vumbi Desemba  17.
  Kwa mujibu wa Meneja wa Kikosi Geofrey Katepa, awali mazoezi hayo yalipangwa ku anza leo lakini kutokana na sababu kadhaa ikiwemo ruhusa kwa baadhi ya wachezaji  ratiba hiyo imesogezwa mbele hadi kesho kutwa.
  “Awali alikuwa tuanze mazoezi leo, kumetokea sababu kadhaa, hivyo tumelazimika kusogeza mbele mpaka siku ya jumatano, wachezaji waliokuwa nje ya jiji la Mbeya wengi  wanawasili leo, na wale amabao wako hapa wamepewa nafasi ya siku moja kukamilisha mambo kadhaa ya kifamilia na kesho wanatakiwa kuripoti kambini tayari kwa kuanza matayarisho ya duru ya pili” alisema Katepa.
  Katika hatua nyingine Meneja Katepa amedokeza kuwa Kocha Mkuu Kinnah Phiri atawasili kesho kutoka nyumbani kwake Mzuzu  nchini Malawi ambako alikwenda kwa mapumziko, huku akisistiza kuwa taarifa za usajili wa dirisha dogo na mambo mengine yote taarifa yake itatolewa  mwishoni mwa mwezi huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WACHEZAJI MBEYA CITY WAANZA KUKUSANYIKA KWA KAMBI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top