• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 30, 2016

  NIGERIA NA CAMEROON 'KOMBE UWANJANI' AWCON 2016

  TIMU ya Nigeria imekwenda fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Afrika Kusini jana mjini Limbe, Nigeria.
  Kwa matokeo hayo, mabingwa hao watetezi watakutana na wenyeji Cameroon Jumamosi katika fainali ambao mapema waliitoa Ghana.
  Shukrani kwake mshambuliaji, Desire Oparanozie aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 54 kuihakikisha timu yake kurudia kucheza fainali kama Windhoek, Namibia, mwaka 2014 ambako Nigeria ilishinda 2-0 kutwaa taji la saba.
  Raissa Feudjio akikimbia kushangilia huku akifuatwa na wenzake baada ya kuifungia Cameroon bao pekee dakika ya 71
  Wachezaji wa Nigeria wakishangilia baada ya Desire Oparanozie kufunga bao pekee dakika ya 54 jana

  Afrika Kusini itamenyana na Ghana kuwania nafasi ya tatu Ijumaa mjini Yaounde, Cameroon.
  Katika mchezo mwingine, wenyeji Cameroon walifanikiwa kutinga fainali baada ya ushindo wa 1-0 dhidi ya Ghana 1-0 jana mjini Yaounde.
  Asante nyingi kwake kiungo Raissa Feudjio aliyefunga bao pekee dakika ya 71 Simba hao wa kike wakiendeleza rekodi yao nzuri katika kuwania taji la kwanza la AWCON.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIGERIA NA CAMEROON 'KOMBE UWANJANI' AWCON 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top