• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 25, 2016

  TEGETE KUAMUA MUSTAKABALI WAKE MWADUI MWAKANI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI mkongwe wa Mwadui FC, Jerry Tegete amesema kwamba ataamua mustakabali wake wa baadaye atakapomaliza Mkataba mwishoni mwa msimu.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online leo, Tegete amesema kwamba kwa sasa anataka kumaliza msimu na mkataba wake kwa ujumla Mwadui FC ndipo afanye maamuzi.
  “Mimi kwa sasa ni mchezaji halali kabisa wa Mwadui FC, na hivi sasa ninajiandaa kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu. Akili yangu kwa sasa nimeielekeza kwenye kucheza Ligi Kuu na kumaliza msimu nipo nifikirie mambo mengine,”amesema.
  Jerry Tegete amesema ataamua mustakabali wake wa baadaye atakapomaliza mkataba Mwadui mwishoni mwa msimu

  Tegete yupo katika mwaka wake wa pili Mwadui FC tangu aondoke Yanga SC mwaka 2014 aliyoichezea tangu mwaka 2007 akitokea sekondari ya Makongo, Dar es Salaam.
  Na wakati mwakani atatimiza miaka 10 tangu aanze kucheza Ligi Kuu, Tegete amesema ndio ataamua mustakabali wake mpya kama kubaki au kuondoka timu ya Shinyanga.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TEGETE KUAMUA MUSTAKABALI WAKE MWADUI MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top