• HABARI MPYA

    Tuesday, March 10, 2015

    SHERMAN AINGILIWA NYUMBANI KWAKE, WEZI WAIBA VITU NA DOLA 2,000 ZA KIMAFRKANI

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa Liberia, Kpah Sherman amekumbana na pigo la aina yake nje ya uwanja kufuatia kibaka mmoja kumuibia kwake.
    Sherman ambaye amepangiwa na klabu yake katika nyumba moja eneo la Shekilango amekutana na pigo hilo jana mchana wakati alipotoka kwake nakuelekea makao makuu ya klabu yake nafasi ambayo kibaka huyo aliitumia.
    Kpah Sherman ameibiwa nyumbani kwake Sinza, Dar es Salaam
    Wezi walitumia kidirisha hiki cha chooni kuingia ndani kuiba

    Sherman ameiambia BIN ZUBEIRY kuwa kibaka huyo alipata nafasi ya kuingia kwake akitumia dirisha la choo cha nyumbani kwake ambapo baada ya kufanikiwa kuingia alifanikiwa kuiba vitu kadhaa vikiwemo kiasi cha fedha Dola za Kimarekani 2,000 (Sh Milioni 3.6) ambazo alikuwa amezihifadhi ndani ya chumba chake humo, viatu mpira jozi mbili pamoja na vifaa vingine vya umeme zikiwemo michezo ya kisasa 'game' na king'amuzi cha DSTV vyenye thamani ya sh Milioni 29.
    Sherman amesema mbali na vitu hivyo pia kibaka huyo pia alichukua baadhi ya nguo zake na bagi lake dogo ambapo tayari ameshatoa taarifa kituo cha Polisi cha Urafiki.
    "Ananijua huyu kibaka ni mtu ambaye tulikuwa tunampa kazi za kufanya hapa katika nyumba zetu alitumia nafasi hiyo wakati nilipotoka tayari nimeshatoa taarifa polisi,"alisema Sherman.
    Hapa ni bafuni, baada ya kuingia kwenda kuiba
    Fedha waliiba hapa pamoja na vitu vingine

    Mwanasheria wa Yanga, Frank Chacha amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo tayari mtuhumiwa ameanza kusakwa taratibu akitajwa kwa jina la Khalid na kupewa kesi namba URP/RB/2245/2015.
    "Tumeshaanza kumsaka mtuhumiwa wa tukio hilo kwa mujibu wa polisi huyu jamaa anaonekana ni kazi yake kufanya uhalifu kwa kuwa tayari alishakuwa na kesi za namna hiyo mbili katika kituo hicho ambazo zoteni za mwaka huu,"alisema Chacha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHERMAN AINGILIWA NYUMBANI KWAKE, WEZI WAIBA VITU NA DOLA 2,000 ZA KIMAFRKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top