• HABARI MPYA

    Wednesday, March 11, 2015

    CANNAVARO HATARINI KUWAKOSA PLATINUM JUMAPILI

    Cannavaro wakati wa kufanyiwa upasuaji jana
    NAHODHA wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ yupo kwenye hatihati ya kuukosa mchezo wa kwanza Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Platinum ya Zimbabwe mwishoni mwa wiki.
    Cannavaro jana alishonwa nyuzi tisa baada ya kuumia Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya mahasimu, Simba SC kufuatia kugongana na kiungo Abdi Banda.
    Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba Cannavaro baada ya kushonwa nyuzi tisa, benchi la ufundi litafuatilia hali yake kama atakuwa tayari kucheza Jumapili dhidi ya Platinum.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CANNAVARO HATARINI KUWAKOSA PLATINUM JUMAPILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top